Akifungua Mafunzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Juma Haji Juma amewataka Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe wao kushiriki kikamilifu katika kusimamia na kuibua vyanzo vya Mapato vilivyopo katika mitaa yao na kuhakikisha hakuna Mapato yanayopotea.
Aidha, Mkurugenzi amewakumbusha Viongozi hao kwamba suala la kusimamia usafi wa Mazingira katika mitaa yao ni ya kwao, hivyo amewataka kwenda kusimamia usafi na kufanya Halmashauri ya Mji wa Bunda kuwa ya mfano kwa usafi.
Mkurugenzi amewataka pia Viongozi wa Serikali za Mitaa kuepuka Rushwa na kwenda kuwahudumia wananchi kwa haki na usawa bila upendeleo.
Baada ya kufungua Mafunzo hayo, Viongozi wa Serikali za Mitaa walipewa mafunzo kutoka kwa Afisa kutoka TAMISEMI pamoja na Wakufunzi kutoka Chuo Cha Serikali za Mitaa Hombolo.
Mafunzo haya yalilenga utendaji kazi wao wa kila siku, kufahamu majukumu, taratibu za manunuzi, namna ya kushughulikia migogoro na mambo mengine mengi ya kiuongozi pamoja na namna bora ya kuibua miradi na vyanzo vya Mapato.
#kaziiendelee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda