Akimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe.Dkt. Vicent Anney, Mkuruenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Bwn. Emmanuel Mkongo amewapongeza wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Kisangwa walio hitimu leo.
Mkongo amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya jitihada nyingi kukiendeleza Chuo hiki ikiwa ni pamoja na kuleta vifaa vya kisasa vya kujifunza na kufundishia, majiko ya gesi kuhakikisha chuo kinatunza mazingira, kuleta fedha kwaajili ya ukarabati wa miundombinu ya chuo na kuongeza kwamba bado serikali inaendelea kukiboresha zaidi chuo hicho.
Aidha Mkongo amesema kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya amezichukua changamoto zote zilizoelezwa na Mkuu wa Chuo na kuahidi kuzifikisha sehemu husika.
Mathalani wakati akikagua kazi za wahitimu Mkurugenzi amewashauri wahitimu hao kwamba ujuzi walioupata wakaunganishe nguvu kwa kuunda vikundi vidogo vidogo na kuanza kazi kwa kutafuta mitaji sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuomba mikopo inayotolewa na Halmashauri.
Awali Mkuu wa Chuo Bwn. Edmund Nzowa amesema Serikali imepunguza kwa kiasi kikubwa Ada ya chuo kutoka laki 5 hadi laki mbili na nusu ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kunufaika. Aidha Mkuu wa Chuo amesema kwa Mwaka huu 2023 jumla ya wanafunzi 558 wamenufaika na mafunzo ya chuo hiki ikiwa hii ni mahafali ya 37 na hivyo kuzalisha nguvu kazi ya kutosha katika Taifa hili.
Mwisho Mkuu wa Chuo amesema lengo la mafunzo wanayotoa katika chuo hicho ni kuwapa vijama stadi mbalimbali za ujuzi ufundi ili waweze kujiajiri kwa kutoa huduma mbalimbali na kujipatia kipato.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda