Kamati ya Lishe ya Halmashauri ya Mji wa Bunda imekutana leo chini ya Mwenyekiti Emmanuel Mkongo Mkurugenzi wa Halmashauri kujadili utekelezaji wa Afua za Lishe kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai - Septemba 2023.
Idara mtambuka zote zinazohusika na lishe zimewasilisha taarifa ya utekelezaji kwa kipindi cha robo ya kwanza na kueleza mipango mkakati ya robo ya pili jinsi watakavyohakikisha afua za lishe zinatekelezwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi mashuleni wanapata chakula chenye virutubisho lishe.
Kikao kimeazimia pia shule zote za msingi na sekondari kupanda miti ya matunda kwa kuanza na matunda ya maembe, mapapai na mapera.
Aidha Mwenyekiti ameendelea kusisitiza Elimu kuendelea kutolewa mashuleni na kwa wazazi na walezi wenye watoto wadogo kuzingatia na kufuata taratibu za lishe bora kwa watoto.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda