Leo tarehe 05.05.2022 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Emmanuel J. Mkongo akiambatana na Afisa Elimu Msingi na Sekondari amekabidhi Kompyuta Tano kwa Mkuu wa Shule ya Sekondari Bunda Mwl. Charles Somba kwaajili ya zoezi la kujifunza na kufundishia ili kuboresha sekta ya Elimu.
Pia, Mkurugenzi amekabidhi mashine ya kudurufu kwa Afisa Elimu Kata Leonard Shoti kwaajili ya matumizi ya Kituo Cha Walimu Balili (TRC).
Vifaa hivi vimetolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kutekeleza Mradi wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa Elimu ya Msingi Awamu ya Pili (GPE - LANES II).
Kupitia mradi huo, Ofisi ya Rais - TAMISEMI imefanya na inaendelea kufanya manunuzi ya vifaa vya TEHAMA vitakavyotumika katika vituo vya Walimu "Teachers resource Centres" kwa lengo la kuviimarisha Ili viweze kutumiwa na Walimu kazini katika kujiendeleza.
#Kaziiendelee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda