Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda Dkt. Vicent N. Anney amezindua bodi ya Afya ya Halmashauri ya Mji wa Bunda leo Jumatano katika ukumbi wa Ofisi yake.
Dkt. Vicent amesema anaimani na bodi ilichaguliwa, aidha ameitaka kutekeleza majukumu yake ya msingi ambayo ni:
Kusimamia huduma ya Afya katika Halmashauri ya Mji wa Bunda, kusimamia miundombinu ya Afya, kubuni vyanzo vya mapato mbalimbali vinavyolenga kuboresha huduma ya Afya na kuongeza pato la Halmashauri, kusimamia uendeshaji wa vituo binafsi vya Afya, kuboresha huduma za iCHF, kusimamia uanzishwaji wa maduka ya dawa baridi yasiyohitajika katika Halmashauri ya Mji, kusimamia hospitali ya Mji wa Bunda kutoa huduma vizuri na majukumu mengine yote yanayohusu bodi.
Awali wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Ndg. Emmanuel Mkongo alisema Bodi hii iliyoundwa itaisaidia Halmashauri kusimamia ufanisi wa shughuli za Afya na kuboresha utoaji wa huduma za Afya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi aliechaguliwa Dkt. Pius Tubeti (mstaafu) alitoa neno la shukrani kwa kuchaguliwa na kuomba ushirikiano kutoka kwa wajumbe wa bodi na watumishi wa Serikali ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya bodi.
Mwisho kwa niaba ya Halmashauri ya Mji wa Bunda Mhe. Mzamil Kilwanila Diwani wa kata ya Bunda Mjini ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya huduma za Jamii Halmashauri ya Mji wa Bunda alimshukuru mgeni rasmi kwa kuzindua bodi hiyo ya afya na kumueleza kwamba majina ya wajumbe hao wa bodi yalipitishwa kwenye baraza la Halmashauri na kuridhiwa na wajumbe wa baraza.
Manthalani, Wajumbe hawa wa bodi kama ilivyoelezwa na Kaimu Mganga Mkuu Dkt. Nuru kwamba wamepatikana baada ya mchakato wa kutuma maombi kukamilika na kati ya walioomba waliokua na sifa ndio waliochaguliwa.
#afyakwanza
#kaziiendelee
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda