Tarehe 18.10.2022
Na Liwina Mnamba
Afisa Mawasiliano Serikalini
Katibu Tawala Wilaya ya Bunda Bw. Salum Mtelela amezindua rasmi maonesho ya juma la Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.
Mtelela ameupongeza Uongozi kwa kuamua kufanya maadhimisho hayo ambayo yalianzishwa na UNESCO mwaka 1966 ambapo Tanzania kwa mara ya kwanza Mwaka 1967 chini ya Uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Kambalage Nyerere.
Katibu Tawala amesema baadae Serikali iliamua kuja na mpango wa MEMKWA (Elimu ya msingi kwa watu waliyoikosa) na MESIKWA (Elimu ya Sekondari kwa watu waliyoikosa). Hata Hivyo Bwana Mtelela amesema watu wasichukulie Elimu hii kama ni jambo la aibu na badala yake watumie fursa hii kuweza kujiendeleza na kwa wale waliokosa fursa ya kuingia katika mfumo rasmi basi waitumie kupata Elimu na maarifa.
Kwa upande wake Mratibu wa Elimu ya watu wazima na Elimu nje ya mfumo rasmi katika Halmashauri ya Mji wa Bunda Mwalimu Maiga ametoa maelezo kwamba Elimu hii ni Ile ambayo watu wote wanapata nje ya mfumo rasmi na Hivyo kuwasaidia watanzania kupata Elimu, maarifa na stadi za maisha Ili kuweza kukabiliana na hali mbalimbali za maisha.
Awali Afisa Tarafa wa tarafa ya Serengeti Bw. Mkangara Mkangara alifanya Utambulisho kwa wageni walioambatana na mgeni rasmi na baadae Afisa Elimu Msingi Mwalimu Said Ramadhan alifanya Utambulisho kwa wageni wote waalikwa.
Maonesho haya yanafanyika katika Viwanja vya shule ya Msingi miembeni na yatadumu kwa muda wa siku mbili ambapo kilele kitakua siku ya Jumatano tarehe 19.10.2022.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda