Leo imekua siku nzuri sana kwa wakazi wa Kata ya Nyamakokoto ambapo Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda imetua katika viwanja vya shule ya Sekondari Nyamakokoto kusikiliza na kutatua kero za wananchi hao.
Wananchi walianza kwa kueleza kero zinazowakabili katika Kata yao ikiwa ni pamoja na ubovu wa Miundombinu ya Barabara, Wizi na udokozi, mifugo kuzurura hovyo mitaani, Walengwa wa Mfuko wa TASAF kulima, eneo la Kilimo Cha umwagiliaji, Mikopo ya asilimia 10 pamoja na Maboresho katika sekta ya Elimu Msingi na Sekondari.
Kwa upande wake Ofisi ya Mkurugenzi iliweza kujibu maswali ya wananchi na kuleta tumaini jipya kwa wananchi hao. Watalamu waliweza kueleza Mipango ya Serikali ikiwa ni pamoja na kukarabati Barabara zilizopo Nyamakokoto, kutoa elimu kuhusu miradi ya TASAF kwamba hawalazimishwi kufanya kazi hizo Bali ni hiari lakini kwasababu inawaongezea kipato watu wanaoishi na mlengwa wenye nguvu wanaruhusiwa kufanya kazi kwa niaba ya mlengwa na fedha zikaingia kwa mlengwa.
Aidha kuhusu Mikopo, Watalamu wameeleza kwamba Serikali ilisitisha kwa lengo la kuangalia namna Bora ya utoaji ili kudhibiti Mikopo kutorejeshwa, kuhusu mifugo kuzurura Afisa Mifugo ameeleza kwamba ni marufuku mifugo kuzurura au kuchungwa mjini kinyume na hapo Sheria itachukua mkondo wake.
Kuhusu Sekta ya Elimu, Afisa Elimu amewaeleza Wananchi kwamba Maboresho yanaendelea na tayari Imeongeza shule ya Sekondari Dokta Nchimbi kuwa na kidato Cha Tano na Sita. Na bado hatua nyingine za maboresho zinaendelea kuchukuliwa.
Bunda Town Council
Anuani ya Posta: 219 Bunda
Sim: +255 28 2621773
Mobile:
Barua Pepe: info@bundatc.go.tz
haki zote zimehifadhiwa.Haki miliki ©2017 Halmashauri ya mji wa bunda